Back to Search View Original Cite This Article

Abstract

<jats:p>Uchanganuzi hakiki wa usemi huwa na haja ya kuunganisha lugha na masuala tatanishi ya kisiasa, kijamii na kitamaduni katika miktadha maalum ya kijamii na kuingilia kati masuala hayo. Makala yamechunguza jukumu la lugha katika kuunda vitambulisho vya kiuana vinavyobadilika kutokana na mahusiano ya uwezo katika jamii. Lengo limekuwa ni kujadili jinsi vipengele vya lugha vinavyosheheni uwezo vimesawiri uana kwa kuzingatia vilongo katika diwani ya Bara Jingine (2001) ambayo imetumiwa kama matini kwa hivyo uchambuzi si wa kifasihi. Tafiti nyingi ambazo zimerejelea diwani hii zimejikita katika wizani, tamathali za usemi, dhamira na maudhui hakuna utafiti ambao umetumia diwani hii kama matini na kuitumia katika uchunguzi wa mahusiano ya uwezo na usawiri wa uana ambao umeangazwa na makala haya. Utafiti umefanyika maktabani na kwenye mtandao ambapo kumekuwa na udurusu wa kazi za wasomi na wataalamu mbalimbali zinazohusiana na makala na ambazo zimepitiwa, kudondolewa na kunakiliwa. Data ya makala imeteuliwa kutoka kwa mashairi matano ya diwani ambayo yana idadi kubwa ya sifa zinazochunguzwa. Mbinu ambayo imetumiwa kuteua sampuli ni ya usampulishaji sinasibu na ya kuchanganua data ni ya uchanganuzi wa matini. Sifa za lugha zimeteuliwa, kugawanywa na kuchunguzwa kupitia mihimili ya nadharia kwa kuzingatia vilongo kwa sababu utafiti ni wa kitaamuli. Makala yameongozwa na nadharia ya uchanganuzi hakiki wa usemi katika mtazamo wa usemi-kihistoria iliyoasisiwa na Wodak na Meyer (2001). Nadharia hii ina mihili minne na inahusika na uchanganuzi wa jinsi tofauti za kijamii na kisiasa zinadhihirika, kuzalishwa na kuendelezwa kupitia usemi kwa kuangaza sifa chanya na hasi za wengine. Makala yameegemea mhimili wa tatu wa nadharia ambao ni wa sifa za kiisimu kama vile nomino, vitenzi na nyingine ambazo zimetumiwa kuangaza mahusiano ya uwezo na usawiri wa uana. Makala yamethibitisha kwamba matumizi ya lugha na usawiri wa uana umeathiriwa na mahusiano ya uwezo ambayo yamejikita katika utamaduni wa jamii..</jats:p>

Show More

Keywords

katika makala lugha uwezo uchanganuzi

Related Articles

PORE

About

Connect