Back to Search View Original Cite This Article

Abstract

<jats:p>Maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa mwaka 2024 nchini Kenya, yaliyoongozwa hasa na vijana wa kizazi cha kisasa (Gen Z), yalionesha kiwango cha juu cha mpangilio na umoja, hali iliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na matumizi ya Kiswahili kama lugha kuu ya mawasiliano na uhamasishaji. Licha ya Kenya kuwa na mandhari ya lugha nyingi, Kiswahili kilijitokeza kama chombo cha kuunganisha kilichovuka mipaka ya kikabila na kieneo na kuwezesha uratibu wa shughuli kupitia majukwaa ya kidijitali, mikutano ya hadhara na kampeni za kijamii. Hata hivyo, kuna utafiti mdogo unaoangazia jukumu la Kiswahili katika kuimarisha mshikamano, ushirikishwaji wa watu wa tabaka mbalimbali na kuhakikisha mafanikio ya harakati kubwa kama hizi. Utafiti huu unalenga kuziba pengo hili kwa kuchunguza jinsi Kiswahili kilivyotumika kama chombo cha kuunganisha na njia ya kimkakati ya mawasiliano wakati wa maandalizi, utekelezaji na matokeo ya maandamano haya. Kupitia uchanganuzi wa jukumu lake, utafiti huu utachangia kuelewa uhusiano kati ya lugha, harakati za kijamii na ushirikiano wa vijana katika muktadha unaoendelea wa kijamii na kisiasa nchini Kenya. Utafiti huu ulitumia mbinu ya uchanganuzi wa kimaelezo ili kuelewa nafasi ya Kiswahili katika harakati za kijamii. Eneo la utafiti lilijumuishavijana wa Jiji la Nairobi. Utafiti ulilenga vijana.  Mbinu ya kusudio ilitumika kuchagua washiriki 200 kutoka katika makundi mbalimbali ya kijamii. Washiriki walijaza hojaji pepe iliyokuwa na maswali yaliyolenga matumizi ya Kiswahili katika uhamasishaji na mshikamano wa kijamii. Matokeo yanaonesha kuwa Kiswahili kilikuwa na nafasi kubwa katika kuondoa vikwazo vya lugha, kushirikisha washiriki wa makundi mbalimbali na kuimarisha mawasiliano kati ya viongozi na jamii. Utafiti huu unatoa mapendekezo ya kuendeleza Kiswahili kama chombo muhimu cha mawasiliano katika mijadala ya kijamii na maendeleo ya kijamii, huku ukijaza pengo lililopo katika tafiti za awali.</jats:p>

Show More

Keywords

kiswahili kijamii katika utafiti kama

Related Articles